Mhe. Waitara akizunugmza na watumishi wa umma katika mkutano wa hadhara
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mheshimiwa Mwita Waitara amesema adhabu kali inayotolewa kwa wanaowapa mimba wanafunzi inalenga kukomesha kabisa tabia hiyo. Mhe. Waitara ametoa kauli hiyo wilayani Newala wakati akizungumza na Wanafunzi,Watumishi wa Umma pamoja na wazazi ikiwa ni mwendelezo wa Ziara yake ya kikazi mkoani hapa.
Amesema mipango ya serikali ni kuweka kipaumbele katika sekta ya Elimu huku ikilenga kila mtoto hususani wanafunzi wa kike kupata fursa ya elimu kama ilivyo sisitizwa katika katiba ya Nchi.
Aidha Mheshimiwa Waitara ambaye ana taaluma ya ualimu amewataka wanafunzi kuweka kipaumbele katika masomo ya Sayansi kulingana na uhitaji wake mkubwa katika jamii.
Nimepita madarasani. nimefundisha somo la hisabati. nimegundua kwamba kuna tatizo la uelewa katika mada za hisabati hivyo walimu wana kazi kubwa kuhakikisha wanafunzi wanafaulu vizuri. Amesema Waitara
Naye afisa elimu Mkoa wa Mtwara Germana Mung’aho amempongeza Mheshimiwa Naibu Waziri na kusisitza kuwa mkoa umejipanga kupambana na changamoto zinazowakabili wanafunzi
Akiwa wilayani Newala Naibu waziri ametembelea Miradi mbalimbali iliyo katika sekta ya Elimu na kushiriki katika kufundisha somo la hisabati katika shule ya sekondari Kiuta.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara
Anuani ya Posta: 544, MTWARA
Simu: +255 23 2333014
Mobile: +255 23 2333014
Barua Pepe: ras@mtwara.go.tz
Haki Miliki © 2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara. Haki zote zimehifadhiwa.