Katibu Tawala Mkoa wa Mtwara Ndg. Abdallah Mohamed Malela amekutana na watumishi wa Sekretarieti ya Mkoa leo tarehe 24/6/2021 kwenye ukumbi wa Boma Mkoa ili kuwahamasisha kuchukua tahadhari dhidi ya ugonjwa wa Corona.
Wataalamu kutoka Seksesheni ya Afya ambao ni Ndg. Serveus Kamala - Afisa Afya na Ndg. Edward Ngonyani - Mratibu wa Maabara Mkoa walitoa elimu ya afya kuhusiana na ugonjwa wa CORONA.
Katika mafunzo hayo watumishi walisisitiziwa kuepuka msongamano wawapo ofisini, kuvaa barakoa wanapokuwa katika mikusanyiko au wakati wa mazungumzo na mtu mwingine, kutakasa mikono, vitasa, meza, milango nk
Na mwisho watumishi wote walikumbushwa kufanya mazoezi, kuzingatia lishe bora na kutoa taarifa pindi waonapo dalili au mshukiwa wa ugonjwa wa CORONA.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara
Anuani ya Posta: 544, MTWARA
Simu: +255 23 2333014
Mobile: +255 23 2333014
Barua Pepe: ras@mtwara.go.tz
Haki Miliki © 2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara. Haki zote zimehifadhiwa.