Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara imeendelea kupokea wawekezaji katika sekta ya zao la korosho. Leo Februari 4, 2019 Mhe. Mkuu wa Mkoa amefanya mazungumzo na Bwana Carl Rehnberg kutoka Sweden.
Bwana Rehnberg ambaye amemtembelea Mhe. Mkuu wa Mkoa ofisini kwake anasema soko lake kubwa la korosho ni nchi za Scandinavia na amekuwa akiipokea korosho toka Tanzania kupitia wafanyabishara mbalimbali wa nje na ndani.
Anasema ameiona fursa kubwa ya kuwekeza katika kiwanda cha kubangua korosho hapa mkoani kwani mazingira yanaruhusu.
Ujio wa wawekezaji wenye sifa hii ni fursa muhimu katika kulipa zao la korosho thamani na kuondokana na wafanyabiashara wa kati.
Wawekezaji wengine waliojitokeza mwaka huu ni pamoja na Mkurugenzi wa makampuni ya IPP Bwana, Reginald Mengi.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara
Anuani ya Posta: 544, MTWARA
Simu: +255 23 2333014
Mobile: +255 23 2333014
Barua Pepe: ras@mtwara.go.tz
Haki Miliki © 2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara. Haki zote zimehifadhiwa.