Mkurugenzi wa Manispaa ya Mtwara Mikindani Beatrice Dominic akimkabidhi Mwenge wa Uhuru Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Mhe. Evod Mmanda wakati wa Mbio za Mwenge wa Uhuru 2017 Mkoani Hapa.
Mbio za Mwenge wa uhuru 2017 zimehitimishwa mkoani hapa juzi na kuacha mengi yenye manufaa. akizungumza Wakati wa kukabidhi Mwenge huo kwa uongozi wa mkoa wa Lindi. Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mheshimiwa Halima Dendego amesema moja ya mazuri yaliyoletwa na mwenge wa Uhuru 2017 ni pamoja na hamasa kubwa katika upimaji wa Virusi vya UKIMWI.
Amesema jumla ya wananchi 2284 walijitokeza kupima maambukizi ya virusi vya UKIMWI wakiwemo wanawake 683 na wanaume1661. Waliogundulika kuwa na virusi vya Ukimwi ni 39 wakiwemo wanaume 19 na wanawake 20 sawa na asilimia 1.7. Aidha katika mkesha wa mwenge uliokuwa ukifanyika kila halmashauri, viongozi walihamasisha matumizi ya kondomu ambapo jumla ya kondomu 7236 za kiume zimegawiwa.
Kwa upande wa uchangiaji damu Dendego amesema wananchi walijitokeza na kuchangia jumla ya unit 135. Aidha suala la mapambano dhidi ya malaria lilipewa msisitizo ambapo wananchi 741 walijitokeza kupima malaria wakiwemo wanaume 509 na wanawake 212. Waliokutwa na vimelea vya malaria ni 101 wakiwemo wanaume 57 na wanawake 44 sawa na asilimia 5.04.
Kwa upande wake kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa, Amour Hamad Amour ameshukuru kwa ushirikiano mzuri walioupata yeye na wenzake kwa kipindi chote cha siku 10 walizokaa mkoani Mtwara.
Amesema yako maagizo mengi waliyoyatoa hapa mkoani na yametekelezwa haraka na kwa Wakati jambo ambalo linampa imani na utendaji mzuri wa viongzoi wa Mkoa wa Mtwara.
Amewataka viongozi wa mkoa kuendeleza umoja huo ili kuendana na falsafa ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa John Joseph Pombe Magufuli ya “Hapa Kazi Tu”.
Mwenge wa Uhuru 2017 uliwasili moani Mtwara tarehe Mei 12 ukitokea mkoani Ruvuma na kukabidhiwa Mkoani Lindi Mei 21.
MWENGE WA UHURU. KARIBU TENA MKOANI MTWARA
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara
Anuani ya Posta: 544, MTWARA
Simu: +255 23 2333014
Mobile: +255 23 2333014
Barua Pepe: ras@mtwara.go.tz
Haki Miliki © 2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara. Haki zote zimehifadhiwa.