Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi Mheshimiwa Japhet Hasunga amesema malipo ya wakulima wa korosho yameanza leo na kwamba hatua hiyo imefikiwa baada ya uhakiki ambao umekamilika kwa vyama vya Msingi 35.
Amesema bado uhakiki unaendelea na kwamba ndani ya wiki mbili watakuwa wamekamilisha na hivyo kila mkulima aliyefiksiha korosho yake sokoni atalipwa fedha yake kwa wakati.
Mheshimiwa Waziri ameyasema hayo jana Novemba 16, 2018 wakati wa kikao chake na waandishi wa habari klilichofanyika kwenye ukumbi mdogo wa Boma ulioko Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara.
Ametahadhalisha baadhi ya wakulima ambao baada ya kuona serikali inanunua korosho kwa bei nzuri wameanza kuingiza korosho za daraja la chini ambazo zilibaki kwenye misimu iliyopita. Amesema korosho hizo tani 20 zimepatikana kwenye ghala la Olam zikiwa zimetokea Chama Cha Msingi Mnyawi kilichoko halmashauri ya Wilaya ya Nanyamba. Pia gunia 5 ambazo zilitokea chama cha Msingi Mbembaleo. Amewataka wananchi kuepuka mambo hayo kwani serikali iko makini na itawabaini wote watakaofanya kinyume na utaratibu.
Vilevile amesema gunia 152 ambazo zilikamatwa zikisafirishwa kutoka nchi jirani ziko chini ya ulinzi na taratibu za kisheria zinaendelea ikiwemo kutaifisha mali hiyo.
AIdha Mheshimiwa Waziri amesema utaratibu wa malipo ya fedha za wakulima ni moja kwa moja kwa wakulima badala ya kuzipitisha kwenye vyama vya msingi. utaratibu huo umechukuliwa ili kufanya zoezi liende kwa haraka na kukamilika kwa wakati.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara
Anuani ya Posta: 544, MTWARA
Simu: +255 23 2333014
Mobile: +255 23 2333014
Barua Pepe: ras@mtwara.go.tz
Haki Miliki © 2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara. Haki zote zimehifadhiwa.