Februali 2019 Mkuu wa Mkoa wa Mtwara aliagiza wakuu wa wilaya wote mkoani Mtwara kuhamasisha kilimo cha ufuta katika maeneo yao ili kuondokana na kutegemea zao la korosho pekee.
Agizo hilo lilienda sambamba na kuzitaka halmashauri kuanzisha mashamba darasa ya ufuta ambayo yaliwekwa chini ya usimamzi wa wataalamu wa Taasisi ya Utafitiwa Kilimo Tanzania Kituo cha Naliendele (TARI-Naliendele)
Halmashauri ziliitikia wito huo kwa kuanzisha mashamba hayo ambayo sasa yanendelea vizuri.
Pia walisimamia wananchi kuanzisha mashamba ya mtu mmoja mmoja, mashamba ya familia na mashamba ya vikundi vya vijana. Baadhi ya mbinu zilizotumika ni pamoja na kuwagawia wakulima mbegu kwa matarajio ya kuwa baada ya kuvuma watarudisha kiasi kilekile walichopewa ili serikali ya eneo husika ikigawe kwa wakulima wengine.
Wakulima walioitikia wito huo wanaanza kuiona dunia inayowezekana kupitia kilimo cha ufuta. Bwala Udede ni mmoja wa wakulima ambaye anataraji kupata zaidi ya milioni kumi ndani miezi miwili ijayo. Msikilize hapo kwenye video hiyo ya dakika mbili tu.
Jeshi la polisi kwa kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na usalama Vimeimarisha ulinzi katika mipaka ya Tanzania ili kuhakikisha wahalifu wanaofanya mauaji na vurugu nchini Msumbiji hawapati nafasi ya kuingia Tanzania.
Hayo yamesemwa leo na Kamishna wa Operesheni na Mafunzo wa Jeshi la Polisi Liberatus Sabas wakati akikagua kikosi maalumu cha kupambana na uhalifu nchini kilichowasili mkoani Mtwara kwa ajili ya kuimarisha ulinzi katika mpaka wa Tanzania na Msumbiji.
Amesema wahalifu hao wamekuwa wakivamia kambi za jeshi, vituo vya polisi, kuchoma moto na kuchukua silaha nchini Msumbiji na pia wameripotiwa kuvamia benki na kupora fedha huko huko Msumbiji.
“Kule hali si shwali kama ambavyo mmekuwa mkisikia kwenye vyombo mbalimbali vya habari. Sisi kwa kutambua hilo, na kutambua umuhimu wa sisi kama Taifa, na umuhimu wa wananchi wa Tanzania kuwa shwali tumejipanga kuhakikisha tatizo hili haliji huku kwetu.”
Amewataka wananchi kutoa ushirikiano kwa kuwasilisha taarifa za mtu yeyote ambaye wanamtilia shaka.
Halmashauri Mtwara kuanzisha kilimo cha Ufuta
Na Evaristy Masuha.
Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mheshimiwa Gelasius Byakanwa ameitaka Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Naliendele kuanzisha mashamba darasa ya ufuta mkoani hapa.
Agizo hilo amelitoa leo wakati akizindua mafunzo ya matumizi sahihi ya viuatilifu kwa wakulima na Maafisa Ugani katika kijiji cha Maili Kumi wilayani Mtwara. Amesema mashamba hayo yatasaidia kutoa elimu kwa wakulima wa ufuta na hivyo kuongeza uzalishaji wa zao hilo. Pia, itapanua uelewa wa teknolojia ya kilimo na kuachana na imani ya baadhi ya wakulima kuwa shamba la ufuta linahitaji kupumzishwa kila baada ya msimu mmoja wa kilimo.
Amezitaja baadhi ya wilaya ambazo zinaweza kuanzishwa mashamba hayo ambayo yatamilikiwa na Halmashauri kuwa ni Masasi, Nanyumbu na Mtwara.
“Dkt. Kapinga, Tunahitaji kuwa na shamba la mfano. Wasiliana na halmashauri ya Masasi tupate shamba kubwa la halmashauri ambalo tutalisimiamia kuonesha kilimo cha ufuta, Pia Nanyumbu na Mtwara.” Amesema Byakanwa.
Amesema ardhi ya kilimo cha ufuta ipo ya kutosha hivyo ni suala la wakulima kuwezeshwa elimu. Amesema kwa sasa mkoa umedhamiria kuendeleza kilimo hicho ambacho kimeingizwa katika mfumo wa stakabadhi ghalani kama ilivyo kwa zao la korosho.
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Naliendelea (TARI–Naliendele) Dkt. Fortunatus Kapinga amesema Taasisi iko tayari kutekeleza agizo hilo. Amesema kilimo cha mazao mbadala imekuwa ni moja ya maekezo yao kwa wakulima wanakapoanzisha mashamba mapya ya korosho hivyo ni suala la kuweka msisitizo na kuongeza elimu zaidi.
Mkoa wa Mtwara ni moja ya wazalishaji wakuu wa zao la korosho ambalo limekuwa likiuzwa kupitia utaratibu wa stakabadhi ghalani. Msimu wa 2019/2020 zao la ufuta pia limeingizwa katika utaratibu huo jambo ambalo linawafanya viongozi wa mkoa kusisitiza kilimo hicho.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara
Anuani ya Posta: 544, MTWARA
Simu: +255 23 2333014
Mobile: +255 23 2333014
Barua Pepe: ras@mtwara.go.tz
Haki Miliki © 2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara. Haki zote zimehifadhiwa.