Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheli Tanzania Dayosisi ya Kusini Mashariki Usharika wa Kanisa Kuu Mtwara, Lukas Mbedule amemtunuku Tuzo ya Mwanamke Jasiri Mkuu wa MKOA wa Mtwara. Mhe. Halima Dendego ikiwa ni kutambua ushupavu wake katika mapambano makubwa anayoyaendesha mkoani Mtwara kutetea rasilimali za mkoa huu kwa manufaa ya jamii nzima.
Akizungumza wakati wa kumkabidhi tuzo hiyo, Askofu Mbedule amesema vipo vielelezo vya mambo mengi makubwa aliyoyafanya Mhe. Dendego ambayo ni kielelezo cha ujasiri wake katika kusimamia haki.
Amesema yeye mwenyewe amekuwa mfuatiliaji wa karibu wa kazi za Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa tangu akiwa Mkuu wa Wilaya ya Tanga kabla ya kuhamishiwa hapa Mtwara miaka mitatu iliyopita.
Akizungumzia hati aliyoitoa Askofu Mbedule amesema hati hiyo inatambulika kama HATI YA ASKOFU YA HESHIMA YA JUU ambayo hutolewa Mara chache, kwa watu wachache hasa baada kujiridhisha na utendaji uliotukuka kwa mhusika.
Maandamano yaliyoambatana na dua maalumu ya kumuombea Rais Magufuli Juni 22, 2017 Mjini Masasi
Wananchi Mtwara wamtaka Magufuli aendelee kuwabana wasafarishaji wa Makinikia
Haki Miliki © 2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara. Haki zote zimehifadhiwa.