Kitengo Cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
Kitengo Cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano kina lengo la kutoa huduma za kitaalamu juu ya matumizi ya teknolojia ya habari na mawasiliano kwa Sekretarieti ya Mkoa, Aidha Kitengo hiki kinaongozwa na Mchambuzi wa Mifumo ya Kompyuta Mkuu ambaye anawajibika kwa Katibu Tawala wa Mkoa.
Majukumu ya Kitengo
Majukumu ya Kitengo cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano:
Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) ni nyenzo muhimu, ambayo mchango wake ni mkubwa katika kuharakisha kufikiwa kwa Malengo ya Milenia ifikapo mwaka 2025. Kukua kwa teknolojia katika Mkoa wa Mtwara, kuna mchango muhimu katika kuhakikisha kuwa wananchi wanapata taarifa kuhusu shughuli mbalimbali za utawala, sera na mipango kwa wakati muafaka, hivyo kuwashirikisha wananchi moja kwa moja katika maamuzi yanayoathiri maisha yao. Kutokana na kuingia kwa utandawazi, dunia sasa imekuwa kama kijiji kimoja tena kidogo sana, kwani mawasiliano yamekuwa yakiboreshwa siku hadi siku na kuwa rahisi
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara
Anuani ya Posta: 544, MTWARA
Simu: +255 23 2333014
Mobile: +255 23 2333014
Barua Pepe: ras@mtwara.go.tz
Haki Miliki © 2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara. Haki zote zimehifadhiwa.