Washiriki wa kozi ndefu ya 13 kutoka chuo cha Taifa cha Ulinzi (NDC) kutoka nchi 16 ikiwemo Tanzania leo tarehe 18 Januari 2025 wamehitimisha ziara yao ya mafunzo mkoani Mtwara.
Akizungumzia umuhimu wa ziara hiyo, kiongozi wa msafara huo Brigedia Jenerali Eric Mhoro ameeleza kuwa washiriki hao wamejifunza mambo mbalimbali ikiwemo kilimo hususan cha korosho pamoja na uzalishaji wa gesi ambayo inanufaisha nchi nzima.
“Masomo yetu yanahusu masuala ya kimkakati kama afya, kilimo, uchumi na mengineyo, maeneo yote ambayo tumetembelea tumeona kwa vitendo vile tulivyokuwa tunajifunza darasani kwamba nchi yetu imepiga hatua kubwa kwenye uzalishaji hasa kwenye kilimo, biashara hata kwenye ajira kwa vijana tumeona jinsi serikali imewawezesha vijana kujiinua kiuchumi. Hata nchi ambazo tunasoma nao pamoja, nao wamejifunza mengi.” Alieleza mmoja wa washiriki wa kozi hiyo Bi. Edith Simtengu
Brigedia Jenerali Mhoro amemshukuru Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Mhe. Kanali Patrick Sawala kwa kuratibu vema ziara yao kwa siku zote nne walizokuwa mkoani hapa.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara
Anuani ya Posta: 544, MTWARA
Simu: +255 23 2333014
Mobile: +255 23 2333014
Barua Pepe: ras@mtwara.go.tz
Haki Miliki © 2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara. Haki zote zimehifadhiwa.