Mkuu wa Wilaya ya Mtwara, Mhe. Abdallah Mwaipaya leo tarehe 06/09/2024 ameripoti rasmi ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mtwara akitokea Wilaya ya Mwanga na kupokelewa na mwenyeji wake Mhe. Kanali Patrick Sawala.
Kufuatia mabadiliko ya kawaida yaliyofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan tarehe 02/09/2024 Mhe. Mwaipaya anachukua nafasi ya Mhe. Mwanahamisi Munkunda aliehamishiwa Wilaya ya Mwanga.
Mkuu wa Mkoa wa Mtwara amemkaribisha Mhe. Mwaipaya na kumhakikishia ushirikiano katika kuendeleza jukumu la kumsaidia kazi Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Kuwatumikia wananchi wa Mtwara.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara
Anuani ya Posta: 544, MTWARA
Simu: +255 23 2333014
Mobile: +255 23 2333014
Barua Pepe: ras@mtwara.go.tz
Haki Miliki © 2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara. Haki zote zimehifadhiwa.