Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Mtwara imempa hati ya pongezi Mhe. Kanali Patrick Sawala, Kamisaa na Mkuu wa Mkoa wa Mtwara kwa Usimamizi, ufuatiliaji na utekelezaji mzuri wa Ilani ya ya Uchaguzi 2020-2025 ya chama hiko.
Mnamo tarehe 7 na 8 Januari 2025 kamati ya siasa mkoa wa Mtwara ilitembelea na kukagua miradi ya maendeleo kwenye Halmashauri zote tisa za mkoa wa Mtwara yenye thamani ya Shilingi Bilioni 98.54 ambapo iliridhishwa na utekelezaji wake.
Kanali Sawala amekabidhiwa hati hiyo ya pongezi leo tarehe 13 Januari 2024 wakati wa kikao cha Halmashauri kuu ya CCM kilichoongozwa na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mtwara, Mwl.Said Nyengedi ambapo pia aliwasilisha taarifa ya utekelezaji Ofisi ya Mkuu wa Mkoa kwa kipindi cha cha kuanzia Januari mpaka Desemba 2024.
“Ofisi ya Mkuu wa Mkoa inawachukulia hatua waendesha maghala wasio waaminifu, wanaocheza na korosho za wakulima kwa kisingizio cha unyaufu. Pia tumeanza kuwachukulia hatua viongozi wa vyama vya msingi wanaochelewesha au kudhulumu malipo ya wakulima.” Alieleza RC Sawala
Aidha, RC Sawala amewaomba viongozi hao kuwahamasisha wanachama wao kulima mazao ya chakula na kujiwekea akiba.
Mwl. Nyengedi amewaambia wajumbe wa kikao hiko kuwa chama bora cha siasa ni kile kinachowaunganisha wananchi na serikali yao, hivyo kuwataka wajumbe hao kushirikiana vema ili kuwaletea maendeleo wananchi.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara
Anuani ya Posta: 544, MTWARA
Simu: +255 23 2333014
Mobile: +255 23 2333014
Barua Pepe: ras@mtwara.go.tz
Haki Miliki © 2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara. Haki zote zimehifadhiwa.