Kiswahili
  • English
  • Kiswahili
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali yaulizwayo mara kwa mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Mtwara Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Mtwara

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Rasilimali watu
      • Elimu
      • Miundo Mbinu
      • Maji
    • Kitengo
      • Huduma za Kisheria
      • TEHAMA
      • Ukaguzi wa ndani
      • Manunuzi
      • Fedha na `Uhasibu
  • Wilaya
    • Mtwara
    • Newala
    • Tandahimba
    • Masasi
    • Nanyumbu
  • Halmashauri
    • MtwaraMC
    • MtwaraDC
    • Tandahimba
    • NewalaDC
    • MasasiDC
    • MasasiTC
    • NanyumbuDC
    • Newalatc
    • NanyambaTC
  • Uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Afya
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Utaratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu za Maombi
    • Profile za Watumishi
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Tukio
  • Ijuwe Mtwara

KAMATI YA BUNGE UWEKEZAJI (PIC) YATEMBELEA MIRADI YA GESI ASILIA MTWARA

Posted on: March 24th, 2024

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma(PIC) imefanya ziara mkoani Mtwara na kutembelea miradi ya gesi iliyopo Msimbati na Madimba. 

Akizungumza katika ziara hiyo Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi TPDC Ombeni Sefue amesema kuwa miradi hiyo ni muhimu kwa taifa ambapo asilimia 65 ya gesi hutumika kuzalishia umeme nchini. 

Amesema kuwa gesi hiyo inatumika kuzalishia umeme nchini ambapo ina mchango mkubwa kwa uchumi wa nchi.

“Tumefarijika kupata fursa ya kuwaonyesha wawakilishi wa wananchi fedha za Taifa hili zinavyotumika na mchango inayotolewa katika uchumi wa nchi kama mlivyosikia asilimia 65 ya umeme unaotumika nchini unatokana na gesi asili ya Songosongo na Mnazibay  tumekabidhiwa jukumu hili kubwa kwa Taifa” amesema Sefue.

Nae Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma Deus Clement Sangu Mbunge wa Jimbo la Kwela Zanzibar amesema kuwa ziara hiyo ni ziara maalum ya kibunge ambayo imeanzia mkoani Tanga katika mradi wa bomba la mafuta. 

“Serikali inafanya kazi kubwa na mabadiliko tumeyaona kwa kiasi kikubwa tunapongeza uwekezaji huo ambapo awali 2019 kulikuwa na wawezekezaji watatu akiwemo TPDC ambapo kwa sasa tumeingia katika rekodi ya nchi ambapo tunamiliki hisa kwa asilimia 40 kwenye miradi ya gesi ambapo 60 zinabakia kuwa za mwekezaji” amesema Sangu.

“Kwenye huu ubia Serikali imeweka zaidi ya shilingi bilioni 104.6 ambapo sasa TPDC anaingia kwenye uzalishaji wenye tija sasa ambapo asilimia 65 inaenda kuzalisha umeme hasa ukizingatia kuwa sasa matumizi yamekuwa makubwa nchini” amesema  Sangu.

Nae Makamu Mwenyekiti wa  Kamati ya PIC Vuma Agustino  amesema kuwa uwepo wa Tanzania kwenye miradi ya  uzalishaji na uchakataji wa gesi asilia nchini unaonyesha kuwa tumepiga hatua kubwa.

“Tunasifu uwepo watanzania hasa vijana kwenye maeneo ambayo tumetembelea yote tumeona watanzania ambapo awali serikali ilikuwa ikitumia fedha nyingi kuwalipa ambayo baada ya serikali kusomesha watanzania na pia nafasi zote zimeweza kuchukuliwa” amesema Augustino.


Machi 24, 2024

#TunaifunguaMtwara

#KaziIendelee

Matangazo

  • MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2024 January 23, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • CSR YAIGUSA JESHI LA POLISI NA UHAMIAJI MTWARA

    April 04, 2025
  • MWENGE WA UHURU 2025 WAWASHWA KIBAHA; KUKIMBIZWA MIKOA 31.

    April 02, 2025
  • RAIS SAMIA ATOA MKONO WA EID NA PASAKA MTWARA

    March 31, 2025
  • RC SAWALA AMUAPISHA DC MASASI; AMPA MAELEKEZO

    March 30, 2025
  • Tazama Zote

Video

"MIRADI YA GESI KUNUFAISHA WAKAZI" MHE. DKT. DOTO BITEKO
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • IKULU
  • UTUMISHI
  • e-GA
  • MAOMBI YA KUCHOMA CHANJO YA UVIKO-19
  • SALARY SLIP
  • NBS
  • TAMISEMI

Kurasa Mashuhuri

  • TOVUTI KUU YA SERIKALI
  • WIZARA YA HABARI
  • TAMISEMI

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Eneo kwa Ramani

Wasiliana Nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara

    Anuani ya Posta: 544, MTWARA

    Simu: +255 23 2333014

    Mobile: +255 23 2333014

    Barua Pepe: ras@mtwara.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali yaulizwayo mara kwa mara
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki © 2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara. Haki zote zimehifadhiwa.