Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Mhe. Kanali Patrick Sawala ameagiza kuundwa kwa timu maalumu itakayokuja na mkakati pamoja na utekelezaji ili kutokomeza malaria ndani ya mkoa wa Mtwara.
Kanali Sawala ametoa agizo hilo leo tarehe 21 Desemba 2024 wakati akiongoza kikao cha Kamati ya Ushauri Mkoa wa Mtwara (RCC) chenye lengo la kujadili utekelezaji wa shughuli mbalimbali za maendeleo.
Taarifa ya afya iliyowasilishwa na Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Dkt. Benedicto Ngaiza imeeleza kuwa Mkoa wa Mtwara bado una kiwango kikubwa cha maambukizi ya ugonjwa wa Malaria ambapo mpaka kufikia Oktoba 2024 maambukizi yameongezeka kwa 20% na kufanya kuwa mkoa wa pili kitaifa katika maambukizi ukiongozwa na mkoa wa Tabora.
Kwa upande mwingine, Mbunge wa Jimbo la Newala Mjini ambae pia ni Waziri wa nchi Ofisi ya Rais, Ikulu (Kazi maalumu), Mhe. George Mkuchika ameshauri mkoa kuunda kamati maalumu itakayoweza kufanikisha Mkoa wa Mtwara kuwa na timu ya mpira wa miguu.
Nae, Mbunge wa Masasi mjini, Mhe. Geofrey Mwambe ameishauri mamlaka ya mapato (TRA) kushirikiana vema na wafanyabiashara na kuwashauri ili namna bora ya kukuza biashara badala ya kusuburi kukusanya kodi tu.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara
Anuani ya Posta: 544, MTWARA
Simu: +255 23 2333014
Mobile: +255 23 2333014
Barua Pepe: ras@mtwara.go.tz
Haki Miliki © 2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara. Haki zote zimehifadhiwa.