Timu ya kampeni ya msaada wa kisheria ya mama Samia kutoka wizara ya katiba na sheria leo tarehe 27 Januari 2025 imekutana na Kamati za Usalama mkoa wa Mtwara na kuwapa mafunzo yatakayowawezesha kuzingatia haki za binadamu na utawala bora.
Akifungua mafunzo hayo, Mkuu wa mkoa wa Mtwara, Mhe. Kanali Patrick Sawala amewataka viongozi hao kuzingatia utawala wa sheria bora.
“Mafunzo haya yatafungua ufahamu wetu wa namna bora ya kushauri na kuongoza watu wetu, ofisi zetu zinatakiwa kuwa msaada na kimbilio kwa wananchi. Sisi viongozi tujiulize tunafanyaje kazi na viongozi wenzetu bila kuingiliana madaraka; tunapaswa tushirikiane.” Aliesema Kanali Sawala
Bi. Juliana Laurent, afisa kutoka Tume ya haki za binadamu na Utawala bora alieleza misingi ya utawala kuwa ni pamoja na uwazi, uwajibikaji, utawala bora, utawala wa sheria, usawa, uadilifu, ufanisi wenye tija, maridhiano, ushirikishaji na mwitikio.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara
Anuani ya Posta: 544, MTWARA
Simu: +255 23 2333014
Mobile: +255 23 2333014
Barua Pepe: ras@mtwara.go.tz
Haki Miliki © 2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara. Haki zote zimehifadhiwa.