Jamii imetakiwa kuzingatia usafi wa kinywa ili kuepuka magonjwa kama matatizo ya afya ya akili, kisukari, mjamzito kujifungua mtoto njiti au mwenye ulemavu hata mimba kuharibika.
Rai hiyo imetolewa mapema leo tarehe 20 March 2025 wakati wa kilele cha maadhimisho ya siku ya afya ya kinywa na meno duniani ambayo kitaifa yamefanyika mkoani Mtwara yakiongozwa na Mhe. Abdallah Mwaipaya, Mkuu wa wilaya ya Mtwara kwa niaba ya Mkuu wa mkoa wa Mtwara.
Mhe. Mwaipaya amewataka wananchi kuzingatia usafi wa kinywa na meno kwa kusafisha mara kwa mara pamoja na kufanya uchunguzi wa kitaalamu walau mara moja kwa mwaka.
“Tabia ya kukata vimeo au kung’oa meno yanayodhaniwa ni ya plastiki husababisha kutokwa na damu nyingi, nitoe wito ni vyema wananchi wakafika hospitalini mara waonapo dalili za matatizo ya kinywa na meno ili kupatiwa ushauri na tiba.” Alieleza Rais wa Chama cha Wataalamu wa Afya ya Kinywa na Meno Tanzania, Dr. Gemma Berege.
Maadhimisho hayo yametanguliwa na wiki ya huduma za matibabu ya meno katika hospitali na vutuo vya afya ndani ya Halmashauri zote 9 zikihusisha huduma za kuziba meno, kung’oa meno, kusafisha meno, upasuaji mkubwa na mdogo wa meno pamoja na kuweka meno bandia.
Kaulimbiu ya maadhimisho hayo inasema “Kinywa chenye furaha, fikra tulivu” iliyotafsiriwa kutoka kiingereza “A happy mouth is, a happy Mind”
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara
Anuani ya Posta: 544, MTWARA
Simu: +255 23 2333014
Mobile: +255 23 2333014
Barua Pepe: ras@mtwara.go.tz
Haki Miliki © 2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara. Haki zote zimehifadhiwa.