Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Kanali Patrick Sawala amesema serikali imewekeza zaidi ya shilingi milioni mia Tano katika miradi mbalimbali katika mwaka wa fedha wa 2024/25 ambazo zimesaidia kuboresha mfumo wa utoaji huduma katika maeneo mbalimbali.
Akizungumza wakati akimkaribisha Mgeni rasmi katika hafla ya uwekaji jiwe la msingi katika mradi wa ujenzi wa vyumba vya madasa katika shule ya msingi Tandika, Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe Stergomena Tax, Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Kanali Patrick Sawala amesema serikali ya awamu ya sita imedhamiria kuwaondolea adha wakazi wa Mtwara katika sekta za afya, elimu, kilimo na maji na hivyo kuwataka wananchi kuunga mkono jitihada hizo Ili ziweze kuwaletea Maendeleo.
Aidha Kanali Sawala amemweleza Waziri Tax kuwa hivi karibuni serikali Kwa kutambua umuhimu wa wakulima wa korosho katika ukanda wa Kusini imewekeza zaidi ya shilingi bilioni 740 kwenye mradi wa makasha ya kupokelea korosho katika msimu mpya wa korosho wa 2024/35 na zaidi ya shilingi bilioni 268 zimewekezwa katika mradi wa barabara ya uchumi ya Mvnivata hadi Masasi huku zaidi ya shilingi bilioni 300 zikiwekezwa kwenye miradi ya Maji.
Kwa upande wake waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe Stergomena Tax amewashukuru wakazi wa Mtwara Kwa kujitolea Kwa hali na mali kufanikisha Miradi ya Maendeleo.
Akizindua Mradi wa zahanati ya Magomeni iliyogharimu zaidi ya shilingi milioni 100 Mhe Tax amesema dhamira ya serikali ya awamu ya sita ni kuona Kila mwananchi anapata huduma zote za kijamii Kwa wakati na Kwa gharama nafuu.
'' Ndugu wananchi na viongozi mliofika kushuhudia tukio hili kwanza naomba niwafikishie salamu za Mhe Rais wetu Dkt Samia Suluhu Hassan, binafsi anasema serikali inatambua changamoto zenu na itaendelea kuzitatua kadri mipango yake na uwezo wa kifedha utakavyoruhusu'' alisisitiza Waziri Tax.
Akiwa katika halmashauri ya Manispaa ya Mtwara Mikindani, Mhe Tax amezindua mradi wa vyumba vya madarasa vilivyo gharimu shilingi milioni 560 ambapo amesema serikali itahakikisha inatatua kero zote zinazowakabili wananchi katika sekta za elimu, afya, maji, barabara na nishati na kuwataka kuitunza miradi hiyo Ili iweze kudumu Kwa muda mrefu.
''Ndugu wanamtwara Kwa kipindi cha miaka mitatu serikali ya awamu ya sita imewalelea zaidi ya shilingi bilioni 700 ambazo zimetumika kutekeleza miradi ya maendeleo, Kwa ujumla hii ni ishara tosha inayodhihirisha upendo wa hali ya juu kutoka Kwa Rais wetu" alisisitiza Waziri Stergomena Tax.
Aidha Mhe Tax amewataka wananchi wanaoishi katika maeneo ilikotekelezwa mirada hiyo ya maendeleo kuwa mabalozi wazurii wanaojivunia miradi hiyo na kuisemea vizuri Ili iwe mfano wa kuigwa katika maeneo mengine.
"Kwa hatua ya maendeleo mliyoifikia Mtwara nawaomba mtembee kifua mbele, waambieni wawekezaji njooni umeme upo wa uhakika, maji yapo pia miundombinu ya usafirishaji ni ya uhakika" aliongeza Mhe Tax.
Kuhusu sekta ya Maji Waziri Tax amesema serikali ya awamu ya sita imefanya kazi kubwa ya kumtua mama ndoo kichwani ambapo Mkoa wa Mtwara Kwa Miaka mitatu mfululizo umepokea mabilioni ya fedha kutekeleza miradi mbalimbali.
"Jamani nikianza kuyaongelea mafanikio tuliyoyapata kupitia utekelezaji wa miradi mbalimbali ya Maendeleo tutakesha, Kwa ujumla itoshe kusema Rais wetu Dkt Samia Suluhu Hassan anafanya kazi kubwa na anastahili kupongezwa" alisisitiza. Waziri Tax.
Naye Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Kanali Patrick Sawala ameitumia fursa hiyo kumshukuru Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan Kwa kuuletea Mkoa wa Mtwara miradi ya mabilioni ya fedha katika sekta za elimu, Kilimo na afya hatua ambayo amesema ni kielelezo cha jitihada za serikali katika kuwasaidia wananchi kujikwamua kiuchumi na kijamii.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara
Anuani ya Posta: 544, MTWARA
Simu: +255 23 2333014
Mobile: +255 23 2333014
Barua Pepe: ras@mtwara.go.tz
Haki Miliki © 2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara. Haki zote zimehifadhiwa.