Katibu Tawala Mkoa wa Mtwara, CPA. Bahati Geuzye amewataka watumishi wa ofisi za Wakuu wa wilaya kufanya kazi kwa bidii na uadilifu pia kutoa huduma bila upendeleo huku wakizingatia matumizi sahihi ya taarifa za ofisi.
Ametoa maagizo hayo siku ya jana tarehe 6 Februari 2025 alipokutana na watumishi wa ofisi za wakuu wa wilaya za Nanyumbu na Masasi kwa lengo za kusikiliza kero na changamoto zinazowakabili.
“Unaweza kuwahi kazini lakini hufanyi kazi, niwatake tufanye kazi kwa bidii pia tujaze taarifa za utendaji kazi kwenye mfumo.” Alieleza CPA. Geuzye.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara
Anuani ya Posta: 544, MTWARA
Simu: +255 23 2333014
Mobile: +255 23 2333014
Barua Pepe: ras@mtwara.go.tz
Haki Miliki © 2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara. Haki zote zimehifadhiwa.