Kiswahili
  • English
  • Kiswahili
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali yaulizwayo mara kwa mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Mtwara Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Mtwara

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Idara
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Mipango na Uratibu
      • Rasilimali watu
      • Elimu
      • Miundo Mbinu
      • Maji
    • Kitengo
      • Huduma za Kisheria
      • TEHAMA
      • Ukaguzi wa ndani
      • Manunuzi
      • Fedha na `Uhasibu
  • Wilaya
    • Mtwara
    • Newala
    • Tandahimba
    • Masasi
    • Nanyumbu
  • Halmashauri
    • MtwaraMC
    • MtwaraDC
    • Tandahimba
    • NewalaDC
    • MasasiDC
    • MasasiTC
    • NanyumbuDC
    • Newalatc
    • NanyambaTC
  • Uwekezaji
  • Huduma
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Afya
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Utaratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu za Maombi
    • Profile za Watumishi
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Tukio
  • Ijuwe Mtwara

UTAFITI WA MIAMBA NA MADINI WAHAMIA MTWARA

Posted on: February 23rd, 2024

Waziri wa Madini Mhe. Anthony Mavunde ameshuhudia jaribio la urushwaji wa Ndege Nyuki (Drone) angani kwa ajili ya utafiti wa miamba na madini hususan madini ya Kinywe, Bati, Shaba, na Chuma katika Kijiji cha Utimbe kata ya Lupaso wilayani Masasi Mkoa wa Mtwara.

Waziri Mavunde ameshudia jaribio hilo leo Februari 23, 2024 baada ya kutembelea eneo linalofanyika utafiti huo kwa lengo la kukagua shughuli za utafiti zinazoendelea katika maeneo mbalimbali nchini ikiwa ni utekelezaji wa Vision 2030 "Madini ni Maisha na Utajiri".

Akizungumza katika eneo la utafiti, Waziri Mavunde amesema mpaka sasa Tanzania ina taarifa za kina za tafiti wa miamba na madini kwa asilimia 16 ambazo zimepelekea uwepo wa migodi mikubwa, ya kati na midogo hivyo amesisitiza kwamba nchi hiyo ikifanyiwa utafiti wa kina wa High Resolution Airborne Geophysical Survey wa angalau asilimia 50 ifikapo 2030  itasaidia ongezeko kubwa la uwekezaji katika Sekta ya Madini.

Aidha, Waziri Mavunde amesema Serikali ya Awamu ya Sita inayo ongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imedhamiria kwa dhati kuhakikisha inawasaidia wachimbaji wadogo wa madini kwa kuwapatia maeneo yenye taarifa za jiolojia ili wachimbe kwa faida na kuondokana na uchimbaji wa kubahatisha.

Awali, Waziri Mavunde alitembelea ofisi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) na ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mtwara kwa lengo la kupata taarifa za shughuli za madini zinazoendelea Mkoani humo.

Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Kanali Ahmed Abbas, ameipongeza Wizara ya Madini kwa kurusha Ndege Nyuki kwa ajili ya utafiti katika eneo lake na pia, amemuomba Waziri Mavunde kusaidia upatikanaji wa soko la madini ya Chumvi sambamba na kujengwa  Kiwanda cha kuchakata madini hayo mkoani humo.

Naye, Mtendaji Mkuu wa GST Dkt. Mussa Budeba amemshukuru Waziri Mavunde kwa kukubali kushiriki na kushuhudia jaribio la urushwaji wa Ndege Nyuki kwa lengo la kufanya utafiti miamba na madini kwa kutumia njia ya teknolojia ya high resolution airborne geophysical survey katika kijiji cha Utimbe wilayani Masasi mkoa wa Mtwara.

Katika tafiti hizo, GST imeshirikiana na Kampuni ya TukuTech Company Ltd kutoka Tanzania, Zanifi Enterprise Ltd kutoka Zambia na Radai OY kutoka nchini Finland kufanya tafiti za miamba na madini katika maeneo mbalimbali nchini kwa kurusha Ndege Nyuki angani kwa kutumia teknolojia ya High Resolution Airborne Geophysical Survey.

Katika hatua nyingine, Dkt. Budeba amesema Ndege Nyuki inauwezo wa kufanya uchunguzi wa madini na miamba katika eneo kubwa kwa haraka ambapo hupelekea kupungua kwa muda na gharama zinazohitajika katika tafiti ikilinganishwa na njia nyingine za utafiti.

Mpaka sasa majaribio ya utafiti wa high resolution airborne geophysical survey unaoendelea kufanyika mkoani Mtwara tayari umefanyika katika mikoa ya Dodoma, Shinyanga, Geita, Manyara na Lindi kwa lengo la kutekeleza dhana ya Vision 2030.


#Vision2030MadininiMaishanaUtajir#

#UtafitiTanzania#

#GeologicalSurveyofTanzania#

#TunaifunguaMtwara

#KaziIendelee

Matangazo

  • MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2024 January 23, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • CSR YAIGUSA JESHI LA POLISI NA UHAMIAJI MTWARA

    April 04, 2025
  • MWENGE WA UHURU 2025 WAWASHWA KIBAHA; KUKIMBIZWA MIKOA 31.

    April 02, 2025
  • RAIS SAMIA ATOA MKONO WA EID NA PASAKA MTWARA

    March 31, 2025
  • RC SAWALA AMUAPISHA DC MASASI; AMPA MAELEKEZO

    March 30, 2025
  • Tazama Zote

Video

"MIRADI YA GESI KUNUFAISHA WAKAZI" MHE. DKT. DOTO BITEKO
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • IKULU
  • UTUMISHI
  • e-GA
  • MAOMBI YA KUCHOMA CHANJO YA UVIKO-19
  • SALARY SLIP
  • NBS
  • TAMISEMI

Kurasa Mashuhuri

  • TOVUTI KUU YA SERIKALI
  • WIZARA YA HABARI
  • TAMISEMI

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Eneo kwa Ramani

Wasiliana Nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara

    Anuani ya Posta: 544, MTWARA

    Simu: +255 23 2333014

    Mobile: +255 23 2333014

    Barua Pepe: ras@mtwara.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali yaulizwayo mara kwa mara
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki © 2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara. Haki zote zimehifadhiwa.