Wajumbe wa Kamati ya Bajeti ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar wamefanya ziara mkoani Mtwara ya kutembelea miradi ya gesi asilia kwa lengo la kujifunza.
Katika ziara hiyo ya siku Moja ambayo wametembelea kiwanda cha kuzalisha gesi Mnazibay pamoja na kiwanda cha kuchakata gesi Madimba.
Akiwakaribisha Mkoani Mtwara Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Mtwara ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Mwanahamis Munkunda amesma kuwa mkoa wa mtwara na lindi unatumia umeme wa gesi asilia pamoja na matumizi ya nyumbani na viwandani.
Amesema uwepo wa gesi hiyo ni fursa kubwa ambayo watajifunza na wataiona.
"Zipo fursa nyingi za uwekezaji mkoani hapa tunakaribisha wawekezaji wengi zaidi mkoa huu ni kitovu cha uwekezaji naimani mtatembea na mtajione" amesema Munkunda.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati ya Bajeti ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mwanaasha Khamis Juma amesema kuwa wamefika mkoani hapa kujifunza katika sekta ya mafuta na gesi asilia .
"Tumekuja kujifunza kwenye miundombinu ya gesi asilia na sisi kwa sasa tunayo mamlaka inayosimamia gesi asilia tumefurahishwa na tumeona maeneo ya kuzalisha na kichakata gesi sisi kama wawakilishi wa wananchi tunaenda kuishauri serikali ili sekta ya gesi iweze kuwa chanzo cha mapato"
Kwa upande wake Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya Mkondo wa Juu Pura
Mussa Ryoba Itumbo (Mjioligia) amesema kuwa ziara hii Ina lengo la kubadilishana uzoefu na kujifunza zaidi.
"Tuna kiasi kingi Cha gesi asilia bado kiko kwenye kina kirefu cha bahari ambapo serikali inafanya mazungumzo na wawekezaji wengine ili wake kuwekeza ambapo kwasasa kuna zaidi ya futi za ujazo 47.13" amesema Itumbo
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara
Anuani ya Posta: 544, MTWARA
Simu: +255 23 2333014
Mobile: +255 23 2333014
Barua Pepe: ras@mtwara.go.tz
Haki Miliki © 2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara. Haki zote zimehifadhiwa.