Watendaji wa Uchaguzi mkoa wa Mtwara leo tarehe 17 Januari 2025 wamekula kiapo cha utii na kutunza siri pamoja na kupatiwa mafunzo kuhusu Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapigakura ikiwa ni maandalizi ya Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025.
Mafunzo haya yamehusisha namna ya ujazaji wa fomu pamoja na kutumia mfumo wa kuandikisha wapiga kura (Voters Registration System - VRS).
Mwenyekiti wa Tume huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji (R) Jacobs Mwambegele alieleza kuwa wakati wa uboreshaji wa Daftari mawakala wa Vyama vya Siasa wataruhusiwa kuwepo katika vituo vya kuandikisha wapiga kura ili kuleta uwazi katika zoezi zima hivyo kupunguza kutokea kwa vurugu zisizokuwa za lazima huku akitoa angalizo la mawakala hao kutowaingia watendaji wakati wote wa utekelezaji wa majukumu yao vituoni.
“Matokeo bora ya zoezi hili yanategemea uwepo wa ushirikiano mkubwa kati ya watendaji wote wa uboreshaji, Serikali, Vyama vya Siasa na wadau wengine wa uchaguzi.” Alieleza Jaji (R) Mwambegele
Aidha, Jaji (R) Mwambegele amesisitiza umuhimu wa utunzaji wa vifaa vya uandikishaji watakavyokabidhiwa, akisema “vifaa hivi vimenunuliwa kwa gharama kubwa sana na vinatarajiwa kutumika katika maeneo mengine ya uandikishaji nchini. Kutokuwa makini katika utunzaji wa vifaa hivi kutapelekea athari kubwa katika ukamilishaji wa zoezi hili muhimu.”
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara
Anuani ya Posta: 544, MTWARA
Simu: +255 23 2333014
Mobile: +255 23 2333014
Barua Pepe: ras@mtwara.go.tz
Haki Miliki © 2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara. Haki zote zimehifadhiwa.