“Bado naendelea kusisitiza vyombo ninavyovisimimia vya Ulinzi na Usalama waendelee kufanya shughuli zao katika maeneo (Mtwara) Kwa sababu tunajua kuna watu ambao tunawatafuta, wamefanya uhalifu katika maeneo yetu, wamekimbilia Msumbiji. Sasa wasije wakatumia fursa hii ya kurudi huku ndani. Lazima tukabe maeneo haya.
Hakuna penati itakayopigwa bila kukabwa. Na anayesimamia chombo chochote kilichoko chini yangu. Ikitokea hawa ambao wanataka kutumia mwanya wa kurudi na baadaye ikabainika ni wahalifu na hawakuwachuja vizuri, basi huyo anayesimamia chombo hicho atapata TAABU SANA. Atapata msukosuko. Iwe ni Jeshi la Polisi. Iwe ni Magereza. Iwe ni Uhamiaji, Zimamoto, Vitambulisho. Watapata TAABU SANA”.
WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI, MHE. KANGI LUGOLA. Julai 18. 2018. Mjini Mtwara.
Mafanikio makubwa katika uzalishaji wa zao la Korosho yaliyopatikana katika kipindi cha awamu ya tano mkoani Mtwara yamewagusa wananchi na sasa wanamtaka Rais Magufuli aendelee kuongoza nchi kwa miaka 30.
Wakulima hao wanadai awam zote za uongozi zlizopita zimefanya mengi mazuri lakini wakulima walikuwa hawajapewa nafasi ya kunufaika na kilimo kama ilivyo sasa.
Bei ya saruji inatarajia kushuka. ajira kuongezeka mara baada ya kumalizika kwa ujenzi wa miundombinu ya kuingiza umeme wa gesi asilia katika kiwanda hicho
Haki Miliki © 2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara. Haki zote zimehifadhiwa.