Mheshimiwa Waziri Mkuu amewaagiza TAKUKURU kufanya uchunguzi juu ya matumizi ya hizo fedha za ujenzi wa jengo la Ofisi za halmashauri hiyo
Ujenzi wa miundombinuya Kituo cha Afya Likombe umefikia asilimia 93 ukiwa umegharimu milioni 326,457,759.18.Kati ya milioni 500 zilizotolewa na serikali kuu kwa kazi hiyo.
Asilimia 7iliyobaki inatarajia kukamilika baada ya wiki mbili kuanzia Januari 1, mwakahuu. Hadi kukamilika mradi huo Manispaa imekadiria kutumia milioni 400 nakubakiwa na shilingi milioni 100.
Mkuu Wa Mkoa wa Mtwara Mheshimiwa Gelasius Byakanwa amefunga mwaka 2017 kwa kupokea mikakati ya utendaji kazi toka kwa wakuu wa Idara na vitengo wa Ofisi Yake. Katika Kikao hicho kilichoafanyika leo Ofisi kwake Mheshimiwa Byakanwa amepokea taarifa za mafanikio na mikakati ya mwaka unaofuata kwa kila Mkuu wa Seksheni na Kitengo na kuwataka kuacha kufanya kazi kwa mazoea.
Mheshimiwa Byakanwa ambaye alichaguliwa kuwa Mkuu wa Mkoa huu hivi karibuni amesema anahitaji kuona Ofisi yake inakuwa na umoja na wote wanafanya kazi kwa ushirikiano.
Awali wakiwasilisha taarifa hizo wakuu wa Idara wameahidi kufanya kazi katika miongozo na maagizo anayoyatoa kama kiongozi wao Mkuu. Aidha wamesema ziko changamoto nyinig lakini zote zina majibu yake ambayo yanawapa matumaini ya kuleta mabadiliko katika idara.
Haki Miliki © 2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara. Haki zote zimehifadhiwa.