Biashara za mipakani kati ya nchi ya Tanzania na Msumbiji zinaenda kuimarika, hii ni kufuatia mabalozi wa nchi hizi mbili kufanya mazungumzo ya kuimarisha usalama, uchumi na mahusiano wa nchi hizi.
Mazungumzo hayo yaliyoitishwa na Mkuu wa mkoa wa Mtwara Mhe. Kanali Patrick Sawala, yamefanyika mapema leo tarehe 27 Februari 2025 yakiwajumuisha Balozi wa Tanzania nchini Msumbiji na Balozi wa Msumbiji nchini Tanzania ikiwa ni hatua ya awali kabla ya kikao cha Ujirani mwema.
Wengine walioshiriki kikao hiko ni Mkuu wa wilaya ya Mtwara Mhe. Abdallah Mwaipaya, maafisa kutoka Wizara ya mambo ya nje, Wizara ya Ofisi ya Rais TAMISEMI pamoja na Kamati ya Usalama mkoa wa Mtwara.
“Nia ya kikao hiki ni kujadiliana namna ya kuimarisha mahusiano ya nchi hizi mbili hususan shughuli za kiuchumi na kiusalama lakini hasa tutapanga siku ya kuwa na kikao cha ujirani mwema.” Alieleza Kanali Sawala
Balozi wa Tanzania nchini Msumbiji ameeleza mahusiano ya kihistoria baina ya nchi hizo mbili hasa wakati wa harakati za kutafuta uhuru wa nchi ya Msumbiji ambapo Tanzania ilishiriki kuwasaidia jambo lililofanya ziwe na mahusiano mazuri mpaka sasa.
“Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan inasisitiza kuimarishwa kwa shughuli za kiuchumi. Jukwaa la ujirani mwema litakuwa ni fursa la kuwezesha nchi hizi kutangaza fursa zake na kuimarisha uchumi wa nchi hizi. Mikoa ya jirani yaani Mtwara na Ruvuma kwa upande wa Tanzania na Cabo Delgado na Niassa nchini Msumbiji mashirikiano yao yatafanikisha maendeleo ya utekelezaji diplomasia ya uchumi.” Alieleza Mhe. Phaustine Kasike, Baloziwa Tanzania Nchini Msumbiji.
Nae Balozi wa Msumbiji nchini Tanzania, Mhe. Ricardo Mtumbaida amepongeza juhudi zinazofanyika kuzidi kuunganisha nchi hizo kiuchumi na kijamii.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara
Anuani ya Posta: 544, MTWARA
Simu: +255 23 2333014
Mobile: +255 23 2333014
Barua Pepe: ras@mtwara.go.tz
Haki Miliki © 2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara. Haki zote zimehifadhiwa.