Mabalozi wa nchi za Msumbiji na Tanzania wakiongozwa na Mkuu wa mkoa wa Mtwara, Mhe. Kanali Patrick Sawala leo tarehe 27 Februari 2025 wametembelea miradi ya maendeleo inayowanufaisha wananchi wa nchi hizo kwa pamoja.
Hatua hiyo imekuja mara baada ya kufanya mazungumzo na kujadili namna ya kuimarisha usalama, uchumi na mahusiano ya nchi hizo mbili hususan maeneo ya mipakani.
Katika ziara hiyo, mabalozi hao walipata nafasi ya kuona kivuko cha Mv Kilambo kitakachokuwa kikifanya safari kati ya Msumbiji na Tanzania katika mpaka wa Kilambo.
Aidha, walipata nafasi ya kutembelea bandari ya Mtwara na hospitali ya rufaa ya kanda ya kusini.
“Hospitali hii imekuwa ni msaada kwa watu wetu wa Msumbiji wanaoishi mpakani hususan jimbo la Cabo Delgado” Alieleza Balozi wa Msumbiji nchini Tanzania, Mhe. Ricardo Mtumbaida
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara
Anuani ya Posta: 544, MTWARA
Simu: +255 23 2333014
Mobile: +255 23 2333014
Barua Pepe: ras@mtwara.go.tz
Haki Miliki © 2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara. Haki zote zimehifadhiwa.