Wilaya ya Mtwara imepakana na Bahari ya Hindi upande wa Mashariki, mkoa wa Lindi upande wa Kaskazini, wilaya ya Tandahimba upande wa Magharibi na nchi ya Msumbiji kwa upande wa Kusini. Wilaya ina eneo la kilometa za mraba 3,760. Aidha kwa wastani eneo kubwa la Wilaya lipo kati ya mita 0 hadi 350 kutoka usawa wa bahari.
Eneo hili kwa sasa limegawanyika katika Halmashauri tatu ambazo ni Halmashauri ya Manispaa ya Mtwara Mikindani yenye kilometa za mraba 163, Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara yenye kilomita za mraba 2,159, Halmashauri ya Mji Nanyamba yenye kilometa za mraba 1,438.
Kwa mujibu wa Sensa ya Watu na Makazi iliyofanyika tarehe 26 mwezi Agosti, Mwaka 2012, Wilaya ilikuwa na jumla ya watu 342,982 wakiwemo wanawake 181,102 na wanaume 161,880. Kufikia mwaka huu 2017, wilaya inakadiriwa kuwa na watu 358,866.
-
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara
Anuani ya Posta: 544, MTWARA
Simu: +255 23 2333014
Mobile: +255 23 2333014
Barua Pepe: ras@mtwara.go.tz
Haki Miliki © 2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara. Haki zote zimehifadhiwa.