Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Mhe. Kanali Patrick Sawala leo tarehe 15 Septemba 2025 amefanya mazungumzo na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Dkt. Charles Edward Kichere ambaye yuko mkoani Mtwara kikazi.
CAG. Kichere amesema ziara yake hiyo ni ya kawaida kwa utendaji kazi kwani Ofisi yake ipo kwenye hatua za Ukaguzi katika Taasisi mbalimbali za umma kabla ya kuwasilisha ripoti kwa Mhe. Rais ifikapo mwezi Machi mwakani.
“Mkuu wa Mkoa nikupongeze kwa usimamizi mzuri kuhakikisha hoja zinafanyiwa kazi, pia niipongeze Ofisi yako kwa ujumla kwa kupata hati safi kwa mwaka uliopita.” Aleleza CAG. Kichere
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara
Anuani ya Posta: 544, MTWARA
Simu: +255 23 2333014
Mobile: +255 23 2333014
Barua Pepe: ras@mtwara.go.tz
Haki Miliki © 2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara. Haki zote zimehifadhiwa.