Mkoa wa Mtwara una Hospitali za Rufaa za Mkoa 2 (Ligula na Ndanda) na Hospitali ya Kanda ambayo ujenzi wa jengo la OPD lenye ghorofa mbili uko kwenye hatua ya umaliziaji.
Hospitali zipo 6 ambapo kati ya hizo Hospitali za wilaya ni 4 zote zikiwa ni za serikali. Jumla ya zahanati zilizopo ni 205 (181 za Serikali) sawa na 34% ya mahitaji ya zahanati katika mkoa. Vituo vya Afya vipo 21 (15 vya Serikali) sawa na 11.9% ya mahitaji. Vituo vya afya 9 vinafanya upasuaji wa dharura.
Zipo changamoto mbalimbali ambazo mkoa unakabiliana nazo. Taarifa kamili ya mkoa hii hapa Taarifa ya utekelezaji wa huduma za afya ustawi wa jamii na lishe_2016.pdf
HOSPITALI YA RUFAA YA MKOA, LIGULA
Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mtwara (Ligula) ilifunguliwa rasmi tarehe 14/10/1964 na Rais wa kwanza wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere. Hospitali hii ilianza na majengo machache yaliyokuwa karibu na mapokezi ya sasa. Wodi ya zamani ya wazazi “Frelimo” ilikuwa ni hospitali ya majeruhi wa chama cha Frelimo ikijulikana kwa jina la “Americo Boavida Hospital”. Kwa sasa wodi hii inafanyiwa ukarabati kwa kushirikiana na Chuo cha Uuguzi Mtwara kutokana na ubovu wa jingo, hivyo jengo jipya la wodi ya wazazi lililojengwa kwa msaada wa shirika la maendeleo la ujerumani (GIZ) ndio linatumia kwa huduma za uzazi. Taarifa kamili ya Hospitali hii hapa TAARIFA FUPI YA HOSPITALI.pdf
KUFANYA MAOMBI YA KUCHOMA CHANJO YA UVIKO-19 (Ugonjwa wa Mlipuko) BOFYA HAPA https://chanjocovid.moh.go.tz/#/
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara
Anuani ya Posta: 544, MTWARA
Simu: +255 23 2333014
Mobile: +255 23 2333014
Barua Pepe: ras@mtwara.go.tz
Haki Miliki © 2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara. Haki zote zimehifadhiwa.