Mkoa wa Mtwara umeibuka kidedea na kushinda tuzo ya Usimamizi bora wa zao la Korosho katika kundi la Sekretarieti za Mikoa ya Asili katika kilimo cha zao la korosho nchini kwa msimu wa mwaka 2024/2025. Tuzo hiyo imepokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Mhe. Kanali Patrick Sawala katika mkutano wa wadau wa tasnia ya korosho uliofanyika mapema leo tarehe 22 Agosti 2025 Jijini Dodoma.
Mkoa wa Mtwara umeibuka kidedea dhidi ya mikoa ya Ruvuma na Lindi ambayo ilikuwa kwenye kinyang’anyiro hicho. Mkoa wa Mtwara umeshinda kwa vigezo vya ongezeko la uzalishaji wa korosho na ongezeko la Ubanguaji wa Korosho. Hii ni mara ya tatu mfululizo kwa mkoa wa Mtwara kushinda tuzo hizo.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara
Anuani ya Posta: 544, MTWARA
Simu: +255 23 2333014
Mobile: +255 23 2333014
Barua Pepe: ras@mtwara.go.tz
Haki Miliki © 2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara. Haki zote zimehifadhiwa.