Wilaya ya Masasi ina ukubwa wa kilometa za Mraba 442,819 sawa na asilimia 23 ya eneo lote la Mkoa wa Mtwara. Inazo Halmashauri mbili. Halmashauri ya Wilaya ya Masasi na Halmashauri ya Mji wa Masasi. Inayo Majimbo matatu ya Uchaguzi ambayo ni jimbo la Masasi, Jimbo la Lulindi na Jimbo la Ndanda.
Kwa mjibu wa sensa ya watu na Makazi ya mwaka 2012, Wilaya ina jumla ya wakazi 377,826 ambapo Halmashauri ya Mji ina wakazi 102,696 na Halmashauri ya Wilaya ina wakazi 275,130. Ongezeko la watu ni 2.7% kwa mwaka.
Wilaya ipo kati ya Longitudo 360 na 380 Mashariki mwa Greenwich na Latitude 100 na 120 Kusini mwa Ikweta . Wilaya inapakana na Wilaya ya Nachingwea kwa upande wa Kaskazini, Wilaya ya Lindi na Newala upande wa Mashariki, Wilaya ya Nanyumbu upande wa Magharibi na Mto Ruvuma upande wa Kusini.
Hali ya hewa ya Wilaya ni joto na baridi kiasi. Miezi ya joto ni Septemba hadi Mei na vipindi vya baridi ni Agosti. Mvua huanza kunyesha mwezi Desemba mpaka Aprili na masika Januari hadi Machi. Wilaya inapata mvua kiasi cha wastani wa mm 893 kwa mwaka na wastani wa joto ni nyuzi joto 250C na kiasi cha juu ni nyuzi joto 320C na kiasi cha chini ni nyuzi joto 220C. pia Wilaya ipo kwenye mwinuko wa Mita 470 toka usawa wa bahari
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara
Anuani ya Posta: 544, MTWARA
Simu: +255 23 2333014
Mobile: +255 23 2333014
Barua Pepe: ras@mtwara.go.tz
Haki Miliki © 2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara. Haki zote zimehifadhiwa.