HISTORIA FUPI YA MKOA WA MTWARA.
Mkoa wa Mtwara ulianzishwa rasmi mwaka 1971 kutokana na Mpango wa Madaraka Mikoani ambao ulilenga kusogeza huduma karibu zaidi na wananchi. Kabla ya hapo mkoa ulikuwa ndani ya Jimbo la Kusini ambalo lilijumuisha Mikoa ya Ruvuma, Lindi na Mtwara ambapo Makao Makuu ya Jimbo yalikuwa Lindi.
Mkoa huu ulipoanzishwa ulikuwa tayari na Wilaya tatu (3) ambazo ni Masasi iliyoanzishwa mwaka 1928 chini ya ukoloni wa Waingereza, Newala mwaka 1956 chini ya wakoloni wa Kiingereza na Mtwara ilianzishwa mwaka 1961. Kutokana na ongezeko la watu na kukua kwa Mkoa wa Mtwara ziliongezeka Wilaya nyingine 2 ambazo ni Wilaya ya Tandahimba iliyoanzishwa mwaka 1995 kutoka kwenye Wilaya ya Newala na Nanyumbu ilianzishwa mwaka 2006 kutoka Wilaya ya Masasi.
Neno Mtwara limetokana na neno la lugha ya Kimakonde “kutwala” ikiwa na maana ya kuchukua (kunyakua) kitu chochote.
KABILA NA UTAMADUNI WA WAKAZI.
Asilimia kubwa ya Wakazi wa asili wa eneo hili ni wamakonde ambao wanatumia lugha ya kimakonde kama nyenzo ya mawasiliano, katika jamii ya kimakonde wamegawanyika katika sehemu mbili, sehemu ya kwanza ni wale wanaoishi katika Ukanda wa Pwani wanajulikana kama ”Wamalaba” na wale wanaoishi tofauti na ukanda wa pwani ” wamakonde wa bara” ingawa wanaongea lugha moja lakini kuna baadhi ya tofauti katika mfumo wao mzima wa maisha katika shughuli za kiuchumi, kijamii na desturi zao. Ukitaka kushuhudia haya unaweza kutembelea maeneo ya pwani kama vile Msangamkuu, Mgao, Nalingu, Msimbati na maeneo mengine yenye asili ya Pwani ambapo utakutana na vitu tofauti na sehemu za bara kama vile Mbawala, Kitere, Dihimba, Nanguruwe pamoja na sehemu zingine za Mtwara Vijijini.
Orodha ya Wakuu wa Mkoa wa Mtwara
kwa maelezo zaidi bonyeza HAPA
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara
Anuani ya Posta: 544, MTWARA
Simu: +255 23 2333014
Mobile: +255 23 2333014
Barua Pepe: ras@mtwara.go.tz
Haki Miliki © 2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara. Haki zote zimehifadhiwa.