Mkuu wa Wilaya ya Newala Mhe. Aziza Mangosongo
Wilaya ya Newala ni moja kati ya wilaya 5 za Mkoa wa Mtwara na ina eneo la Kilomita za mraba 2,439. Kiutawala Wilaya imegawanyika katika Halmashauri 2 ambazo ni Halmashauri ya Mji wa Newala na Halmashauri ya Wilaya ya Newala. Inazo Tarafa 6. Kata 38. Vijiji 26 na Vitongoji 189 zinazounda Halmashauri ya Mji Newala na Kata 22, Vijiji 107 na Vitongoji 303 vinavyounda Halmashauri ya Wilaya Newala. Wilaya pia ina majimbo 2 ya uchaguzi ya Newala Mjini na Newala Vijijini.
Wilaya hii ipo Kusini Mashariki mwa Tanzania. Inapakana na Wilaya ya Lindi Vijijini kwa upande wa Kaskazini, Wilaya ya Tandahimba upande wa Mashariki, Wilaya ya Masasi upande wa Magharibi. Kwa upande wa Kusini Wilaya ya Newala inapakana na Jamhuri ya Watu wa Msumbiji.
Wilaya ipo kati ya nyuzi 390 – 400 Mashariki na nyuzi 100 – 110 Kusini mwa Ikweta.
Wilaya ya Newala iko katika maporomoko ya Makonde yenye mwinuko wa mita 200-900 kutoka usawa wa bahari na ina ukubwa wa eneo la kilometa za mraba 2,439. Eneo linalofaa kwa kilimo ni Ha 196,000. Eneo la malisho ni Ha 51, 400. Eneo la Umwagiliagi ni Ha 2,100 na eneo la Hifadhi ya Misitu ni Ha 1,500. Umbali kutoka Makao Makuu ya wilaya hadi Mtwara mjini kwa njia ya barabara ni Km.166.
SHUGHULI ZA KIUCHUMI
Asilimia 97% ya wakazi wa Newala wanajishughulisha na Kilimo pamoja na Ufugaji wakati asilimia 3 ni wafanyabiashara na Watumishi.
Wastani wa pato la mwananchi wa Wilaya ya Newala ni Tshs 569,736/= kwa mwaka. Wastani huu umezingatia mapato yanayotokana na uzalishaji wa mazao ya Kilimo kama vile Korosho kama Zao Kuu la Biashara. Mazao mengine ni Karanga, Njugu, Mbaazi, Mpunga na Mahindi n.k. ambayo wakulima wanayatumia kama zao la chakula na ziada huuza ili kujiongezea kipato.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara
Anuani ya Posta: 544, MTWARA
Simu: +255 23 2333014
Mobile: +255 23 2333014
Barua Pepe: ras@mtwara.go.tz
Haki Miliki © 2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara. Haki zote zimehifadhiwa.