Wilaya ya Tandahimba inapakana na Wilaya ya Newala kwa upande wa magharibi, Wilaya ya Mtwara upande wa mashariki, Mkoa wa Lindi upande wa Kaskazini na Mto Ruvuma upande wa Kusini ambao ni mpaka Rasmi na nchi ya Msumbijji.
Wilaya ina eneo la kilomita za mraba 1,673,31. Kati ya hizo kilomita za mraba 1,573,04 zinafaa kwa kilimo na ufugaji.
Wilaya ina miji midogo miwili ya Tandahimba na Mahuta, Tarafa 3 za Litehu, Namikupa na Mahuta, Kata 32, Vijiji 143, Vitongozji 654 na Jimbo moja la uchaguzi.
Kwa mjibu wa sensa ya watu na makazi ya mwaka 2012 wilaya ilikuwa na wakazi 2227,901 (wanawake 130,456 na wanaume 112,445). Kati ya watu wote, wilaya inakadiriwa kuwa na nguvu kazi ya wananchi 87,777 (wanawake 50,079 na wanaume 37,698).
Wastani wa pato la wilaya (GDP-Provisional) kwa mwaka 2015/2016 ilikuwa ni Bilioni 134.42 na katika kipindi cha 2016/2017 pato la wilaya limeongezeka hadi kufikia Bilioni 280.41 kutokana na uzalishaji wa mazao ya biashara hasa korosho pamoja na mzunguko wa fedha za wananchi.
Wastani wa Pato la mwananchi kwa mwaka wa fedha 2015/2016 katika wilaya lilikuwa shilingi (GDP 563,312/= Per Capital Income). Katika kipindi cha mwaka 2017/2018 pato la mwananchi linakadiriwa kufikia shilingi 1,154,440.2 kutokana na uzalishaji wa korosho
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara
Anuani ya Posta: 544, MTWARA
Simu: +255 23 2333014
Mobile: +255 23 2333014
Barua Pepe: ras@mtwara.go.tz
Haki Miliki © 2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara. Haki zote zimehifadhiwa.