Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Mhe. Kanali Patrick Sawala leo tarehe 10 Septemba 2025 ametoa rai kwa wana habari kutumia vema kalamu zao katika kutoa taarifa kwa umma.
“Niwapongeze kwa kazi nzuri ya kuuhabarisha umma. Mwana habari ni kiongozi, kupitia kalamu yako una nguvu ya kuunganisha umma. Niwasihi kutumia kalamu zenu vizuri na kutafakari matokeo ya habari kabla hujaamua kuitoa kwa umma.” Alieleza Kanali Sawala
Aidha, ametoa rai kwa wana habari hao kutangaza fursa mbalimbali zinazopatikana ndani ya mkoa wa Mtwara ili wananchi waweze kuwekeza. Pia kuutangaza vema utalii na vivutio.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara
Anuani ya Posta: 544, MTWARA
Simu: +255 23 2333014
Mobile: +255 23 2333014
Barua Pepe: ras@mtwara.go.tz
Haki Miliki © 2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara. Haki zote zimehifadhiwa.