Katibu Tawala Mkoa wa Mtwara, CPA. Bahati Geuzye mapema leo tarehe 30 Mei 2025 ameongoza kikao cha kamati ya lishe Mkoa kilichojadili hali ya utekelezaji wa Afua Jumuishi za Lishe kutoka Idara na Taasisi mbalimbali kwa kipindi cha mwezi Januari-Machi 2025 katika mkoa wa Mtwara.
Miongoni mwa mambo yaliyojadiliwa ni pamoja na hali ya utoaji wa huduma za lishe kwenye vituo vya kutolea huduma za afya, hali ya utoaji wa huduma za lishe kwenye jamii, hali ya uwepo wa chakula katika kaya, hali ya utoaji wa chakula shuleni, hali ya uchanganyaji wa chumvi na madini joto na hali ya urutubishaji wa chakula.
Vikao vya kamati ya Lishe vina lengo la kuimarisha hali ya Lishe kwa wananchi na kutokomeza matatizo ya Lishe ndani ya Mkoa wa Mtwara.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara
Anuani ya Posta: 544, MTWARA
Simu: +255 23 2333014
Mobile: +255 23 2333014
Barua Pepe: ras@mtwara.go.tz
Haki Miliki © 2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara. Haki zote zimehifadhiwa.