Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mhe. Kanali Patrick Sawala amewaagiza Waheshimiwa Wakuu wa wilaya za Mtwara kusimamia kikamilifu zoezi la utambuzi wa wakulima ambao hawakupata ruzuku ya pembejeo ili waweze kupatiwa viwatilifu hivyo.
Kanali Sawala ametoa agiza leo tarehe 08 Julai alipokuwa akiongoza kikao cha kujadili hali ya usambazaji pembejeo mkoani Mtwara kilichofanyika katika ukumbi wa Boma.
“Kuna wakulima hawajapata pembejeo, twendeni mashambani tukaone hali halisi kila mkulima apate anachostahili. Ninatoa siku 10 zoezi hilo liwe limefanyika.” Alisema Kanali Sawala
Aidha Kanali Sawala amewataka maafisa ushirika na maafisa kilimo kutoa elimu kwa wakulima kuhusu matumizi sahihi ya viwatilifu ili pembejeo zinazotolewa na Serikali ziwasaidie kupata matokeo bora.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Korosho Tanzania, Ndg. Francis Alfred ameeleza kuwa watachukua hatua za kisheria kwa watendaji watakaofanya udanganyifu kwenye mifumo na kwa mkulima atakaetoa pesa ili apate pembejeo nyingi.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara
Anuani ya Posta: 544, MTWARA
Simu: +255 23 2333014
Mobile: +255 23 2333014
Barua Pepe: ras@mtwara.go.tz
Haki Miliki © 2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara. Haki zote zimehifadhiwa.