Kampeni ya kitaifa ya chanjo kwa mifugo na utambuzi wa mifugo iliyopatiwa chanjo yazinduliwa mkoani Mtwara leo tarehe 05 Julai 2025.
Akizindua kampeni hiyo Katibu Mkuu Wizara ya mifugo na uvuvi, Bi. Agnes Kisaka Meena ameeleza kuwa Serikali itatoa chanjo bure kwa mifugo aina kuku na kwa mifugo aina ya ng’ombe na mbuzi Serikali imetoa ruzuku ya asilimia 50 ambapo mfugaji atachangia shilingi 500 kwa chanjo.
Katibu Tawala Mkoa wa Mtwara, CPA. Bahati Geuzye amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwajali wafugaji na kuwaletea chanjo za mifugo huku akiahidi kusimamia vema zoezi hilo la uchanjaji kwa mkoa wa Mtwara ili liweze kufanikiwa.
Kampeni hiyo kitaifa ilizinduliwa na Mhe. Rais Samia huko Bariadi mkoani Simiyu Juni 16, 2025 ikielezwa kuwa zoezi la chanjo na utambuzi wa mifugo iliyopata chanjo litakuwa ni endelevu kwa miaka mitano.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara
Anuani ya Posta: 544, MTWARA
Simu: +255 23 2333014
Mobile: +255 23 2333014
Barua Pepe: ras@mtwara.go.tz
Haki Miliki © 2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara. Haki zote zimehifadhiwa.