Mkuu wa mkoa wa Mtwara Mhe Gelasius Byakanwa akisisitiza jambo wakati wa kikao cha Tathimini ya utekelezaji wa mkataba wa afua za lishe Mkoani Mtwara
Maafisa Lishe mkoani Mtwara wametakiwa kuhakikisha wanatoa elimu ya lishe kwa jamii ili kuondokana na maradhi yanayotokana na ukosefu wa chakula bora. Agizo hilo limetolewa na Mkuu wa Mkoa huo Mheshimiwa Gelasius Byakanwa wakati wa kikao cha tathimini ya utekelezaji wa afua za Lishe kilicho fanyika katika ukumbi wa Boma Mkoani hap. Amesema zipo changamoto ambazo zinawakumba jamii kutokana na ukosefu wa elimu hivyo maafisa wa lishe wakijikita katika kuifikia jamii hiyo changamoto hizo zitaondoka.
Akirejea tafiti za takwimu za hali ya lishe mkoani hapo amesema takribani Watoto 67,109 wamedumaa kutokana na lishe duni. Aidha, watoto 139, 981 wanaupungufu wa damu mwilini.
Katika kikao hicho kilichowahusisha viongozi mbalimbali wa mkoa huo wakiwemo wakuu wa wilaya, wakurugenzi na Maafisa wa lishe amewataka kujipanga ili siku moja wakutane kwa ajili ya mazoezi ya viungo ambayo ni mojawapo ya njia za kuboresha afya. Aidha baada ya mazoezi hayo wajitolee kuchangia damu.
Kikao hicho kimefanyika ikiwa ni muendelezo wa vikao mbalimbali vyenye lengo la kutathimini njia bora ya kuhakikisha jamii inaondokana na magonjwa yanayotokana na lishe duni.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara
Anuani ya Posta: 544, MTWARA
Simu: +255 23 2333014
Mobile: +255 23 2333014
Barua Pepe: ras@mtwara.go.tz
Haki Miliki © 2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara. Haki zote zimehifadhiwa.