Kufuatia mabadiliko ya nafasi mbalimbali za uongozi yaliyofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan siku ya tarehe 23 Juni 2025, mkoa wa Mtwara uliguswa na mabadiliko hayo.
Katibu Tawala wilaya ya Mtwara, Bw. Richard Jackson Mwalingo amechukua nafasi ya Mhe. Mwinyi Ahmed Mwinyi aliyeteuliwa kuwa Mkuu wa wilaya ya Arumeru; Bi Zainab Salum Mgomi ameteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Nanyamba akichukua nafasi ya Mhandisi Mshamu Ali Munde aliyestaafu.
Kwa pamoja Bw. Mwalingo na Bi. Zainab leo tarehe 27 Juni 2025 wamefika Ofisi ya Katibu Tawala Mkoa wa Mtwara kuripoti tayari kwa kuanza majukumu yao mapya ya kazi.
Katibu Tawala Mkoa wa Mtwara, CPA. Bahati Geuzye amewahakikishia ushirikiano huku akiwataka wakasimamie miradi ya maendeleo na kuhakikisha mapato yanakusanywa ipasavyo.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara
Anuani ya Posta: 544, MTWARA
Simu: +255 23 2333014
Mobile: +255 23 2333014
Barua Pepe: ras@mtwara.go.tz
Haki Miliki © 2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara. Haki zote zimehifadhiwa.