Ziara ya kidiplomasia ya uchumi iliyofanywa na Kaimu Balozi wa Marekani nchini Tanzania, Andrew Lentz leo tarehe 30 Juni 2025 imeonesha kufungua milango ya ushirikiano baina ya nchi hizi mbili na fursa za uwekezaji kwa raia wa Marekani.
Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Mhe. Kanali Patrick Sawala amepongeza jitihada zinazofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kuitangaza Tanzania kimataifa hali iliyopelekea mataifa hayo kupitia Balozi zao nchini kutafuta fursa za uwekezaji kwa raia wa nchi zao.
Kaimu Balozi Lentz alipata fursa ya kutembelea bandari ya Mtwara ambapo ameonesha kuvutiwa na uwekezaji mkubwa uliofanyika wa kujenga gati jipya lenye uwezo wa kupokea meli kubwa na kuhudumia shehena nyingi zaidi.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara
Anuani ya Posta: 544, MTWARA
Simu: +255 23 2333014
Mobile: +255 23 2333014
Barua Pepe: ras@mtwara.go.tz
Haki Miliki © 2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara. Haki zote zimehifadhiwa.