Kamishna wa Oparesheni na mafunzo wa Jeshi la Polisi Tanzania, CP. Awadhi Juma Haji akiambatana na Wakuu wa Polisi wa Wilaya (OCD) zinazopitiwa na miundombinu ya gesi asilia itokayo Msimbati (Mtwara) kwenda Dar es Salaam kupitia mikoa ya Lindi na Pwani pamoja na viongozi wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) wamefika mkoani Mtwara kwa lengo la kuona na kukagua miundombinu ya gesi asilia.
Akizungumza wakati wa kikao kilichofanyika katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mtwara mapema leo tarehe 20 Mei 2025, CP. Awadhi ameeleza kuwa ziara hiyo ni ya kawaida na hufanyika kila mwaka kwa lengo la kufanya tathmini ili kuboresha miundombinu hiyo.
CP. Awadhi ametumia nafasi hiyo kutoa rai kwa Maafisa wa Jeshi la Polisi kujitokeza kujiandikisha na kuboresha taarifa zao katika Daftari la mpiga kura, zoezi linaloendelea katika mkoa Mtwara mpaka tarehe 22 Mei 2025, huku akisisitiza kuwa kupiga kura ni haki ya kila Mtanzania.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara
Anuani ya Posta: 544, MTWARA
Simu: +255 23 2333014
Mobile: +255 23 2333014
Barua Pepe: ras@mtwara.go.tz
Haki Miliki © 2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara. Haki zote zimehifadhiwa.