Mbio za Mwenge wa Uhuru 2018 zimekamilisha ziara yake katika Halmashauri ya wilayani Masasi tayari kuelekea Halmashauri ya Mji wa Newala. Akiwasilisha taarifa ya Mbio za Mwenge katika Halmashauri, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Masasi, Bi, Changwa Mkwazu amesema Mwenge wa Uhuru 2018 umeacha mafanikio makubwa wilayani Masasi. Ametaja baadhi ya mafanikio hayo kuwa ni pamoja na kujenga umoja na mshikamano wa wanaMasasi.
Kwa upande wa miradi iliyopitiwa na Mwenge huo uliozinduliwa tangu mwaka 1961 na Baba wa Taifa Mwl. Julius Kambarage Nyerere amesema jumla ya miaradi 6 ambapo miradi 4 imewekewa mawe ya Msingi, mradi mmoja umezinduliwa wakati mradi mmoja ulikuwa wa kutoa hundi za mikopo kwa vikundi vya wanawake na vijana. Thamani ya miradi yote ni shilingi 2,406,699,000/=.
Kwa upande ake Mkuu wa Wilaya ya Newala ameupokea Mwenge huo huku akiahidi kuulinda hadi mwisho wa mbio hizo.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara
Anuani ya Posta: 544, MTWARA
Simu: +255 23 2333014
Mobile: +255 23 2333014
Barua Pepe: ras@mtwara.go.tz
Haki Miliki © 2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara. Haki zote zimehifadhiwa.