Afisa Elimu Mkoa, Germana Mung'aho akimuonesha Mkuu wa Mkoa Baadhi ya Vikombe vya mashindano ya UMISETA na UMITAMSHUMTA vilivyoletwa na wanafunzi wa Mkoa wa Mtwara katika mashindano yaliyofanyika kitaifa 2018 mjini Mwanza.
Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mheshimiwa Gelasius Byakanwa amewataka Wakurugenzi na Wakuu wa Wilaya kuhakikisha katika mipango yao ya ujenzi wa shule za kidato cha sita wanajenga shule za Mchepuo wa sayansi. Amesema kwa kuanzisha shule za mchepuo huo kutawavutia wanafunzi wengine kusoma masomo hayo kutokana na hamasa ya wenzao. Pia itasaidia kuondoa tatizo la walimu wa masomo hayo. kinachotakiwa ni viongozi kudhamiria na kuhakikisha mahitaji yote ya ujenzi wa shule zenye sifa hizo wanayatekeleza.
Kwa upande wa vyumba vya madarasa, amesema wameanza na utatuzi wa tatizo hilo katika Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara ambapo shule 10 ambazo wanafunzi wake walikuwa wanasomea chini ya miti zimejengewa vyumba vya madarasa, Ameagiza kila Mkurugenzi ahakikishe anaondoa changamoto hiyo katika eneo lake.
Vilevile amepiga marufuku kusajili shule ambazo hazina vigezo. Ameeleza kuwa mapungufu mengi ya vyumba vya madarasa na ofisi za walimu yametokana na wenye jukumu la usajili wa shule hizo kutofuata vigezo. Amewataka wasikubali kushinikizwa na wanasiasa kwa matamanio yao ya kisiasa.
Bonyeza HAPA kupata picha na maelezo zaidi
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara
Anuani ya Posta: 544, MTWARA
Simu: +255 23 2333014
Mobile: +255 23 2333014
Barua Pepe: ras@mtwara.go.tz
Haki Miliki © 2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara. Haki zote zimehifadhiwa.