Na Michael Bakiri -
Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Brigedia Jenerali Marco Gaguti, amewapongeza viongozi na wananchi wa Mtwara kwa mapokeo mazuri ya chanjo ya UVIKO 19 katika mkoa huo, Mkoa wa Mtwara hadi kufikia siku ya leo umekuwa mstari wa mbele kwa kufikia asilimia 85 ya chanjo ya UVIKO 19 kati ya dozi 20,000 ilizokuwa zimepokelewa tokea Julai, 28,2021 kwenyeMkoa huo.
Amesema kuwa, katika kuhakikisha asilimia 15 za dozi zilizobaki zinakamilika fursa za chanjo zitolewe kwa wananchi hususani kwa maeneo ambayo yalibainika kuwa chini katika uchanjaji.
Katika kufanikisha zoezi hilo Gaguti amesisitiza kuwa, katika zoezi Shirikishi na Harakishi linalo endeshwa na Serikali kwa sasa, ni vizuri kila mtu ambaye bado hajajitokeza, aweze kujitokeza apate elimu na akielimika aweze kupatiwa chanjo ya UVIKO 19.
Mhe. Gaguti amewataka wadau kuendelea kutoa elimu kwa njia mbalimbali kupitia vikao vya kamati za msingi vya afya, kwenye Halmashauri, sambamba na kwenda kwa wananchi kufanya mikutano vijiji na Mitaa, kutoa ufafanuzi na maelekezo sahihi kwenye sinto fahamu kwa baadhi ya makundi ya watu.
“Kuanzia tarehe 01 Oktoba 2021 wataalam wapite nyumba kwa nyumba na maeneo yenye mikusanyiko sokoni, stendi na sehemu zinazotoa huduma mbalimbali ikiwepo kwenye Misikiti na makanisa kwa siku za ijumaa na jumapili na kutoa huduma za chanjo kabla na baada ya ibada, huku wakizingatia namna rahisi ya utoajiwa chanjo kwa haraka bila ya foleni ili kurahisisha zoezi hilo.
Mhe. Gaguti amewataka wananchi kujitokeza kwa wingi kupata chanjo ya UVIKO 19 jambo ambalo litawezesha wananchi wengi kupata chanjo na kufanya kazi zao kwa uhuru bila ya woga wa virusi vya UVIKO.
Pichani: Mhe. Brigedia Jenerali Marco Gaguti (Kushoto) pamoja na Katibu Tawala Ndg. Abdallah Mohamed Malela (Kulia)
wakati wa kikao cha Kamati ya Afya ya Msingi, Kilichofanyika ukumbi wa Boma uliopo Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Leo.
Wajumbe kamati ya Ulinzi na Usalama
Wakuu wa Wilaya
Washiriki na Wadau mbalimbali
# Mtwara bila ya UVIKO inawezekana
#Ujanja Kuchanja.
#Kilammoja atimize wajibu wake.
#MTWARA KUCHELE
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara
Anuani ya Posta: 544, MTWARA
Simu: +255 23 2333014
Mobile: +255 23 2333014
Barua Pepe: ras@mtwara.go.tz
Haki Miliki © 2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara. Haki zote zimehifadhiwa.