Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mhe. Gelasius Byakanwaamewataka waajili wote mkoani Mtwara kuhakikisha wanajari maslahi yawafanyakazi na kuhakikisha wanawatunuku vyeti vya ubora kulingana na utendaji kaziwao. Amesema anazo taarifa za baadhi ya taasisi kutoa zawadi za ufanyakazi borakwa ratiba bila kuzingatia utendaji kazi.
“Haiwezekani mfanyakazi bora akapatikana kwaratiba. Hiyo haiwezei kuchochea utendaji kazi.” Amesema Byakanwa
Kauli hiyo ameitoa jana wakati wa maadhimisho yasiku ya wafanyakazi duniani ambayo kimkoa yamefanyika mjini Masasi.
Aidha, amewataka wafanyakazi kuwa na umojaunaosimamia maslahi yao kwa kutumia utaratibu mzuri wa kuwasilisha madai yaokwa Serikali kwani Serikali ni sikivu na inajali maslahi ya wafanyakazi naimejipanga kuyaboresha kadri uchumi unavyoimarika.
Amewaeleza wafanyakazi kuwa, kauli mbiu ya sikuya wafanyakazi mwaka huu 2019, inavyosema nchi haiwezi kufika katika uchumi waviwanda na uchumi wa kati kama hawapo wafanyakazi wenye maslahi bora na amewahakikishiawafanyakazi kuwa maombi na mawazo yao yote yamechukuliwa na yatafanyiwa kazi.
Kwa upande wao, wafanyakazi waliiomba Serikalikupitia viwango vya mishahara ya wafanyakazi wa umma na sekta binafsi nakuja na viwango vipya kwa kuwa viwango vilivyopo sasa havikidhi mahitajiukilinganisha na kupanda kwa gharama halisi za maisha za sasa; waliipongezaSerikali kwa kulipa madeni yanayotokana na mishahara, likizo, uhamisho,matibabu na masomo na kuondoa au kupunguza madeni ya watumishi yasiyokuwa yalazima. Hata hivyo waliomba madeni yaliyohakikiwa yalipwe ili kuongeza moraliya kufanya kazi kwa ufanisi mkubwa.
Pia watumishi waliendelea kuiomba Serikalikuwapandisha madaraja kwa wakati na kurekebishiwa mishahara yao kulingana namadaraja mapya waliyonayo; kuwekwa kwa mazingira yanayovutia ya uwekezaji waviwanda vidogo vidogo ili kuwapa wananchi fursa ya kupata ajira; na Serikalikuongeza idadi ya wafanyakazi kwenye vituo vipya vya afya na hospitali zawilaya ili kuboresha zaidi huduma za afya.
Kauli mbiu ya siku ya wafanyakazi kwa mwaka 2019ni ‘Tanzania ya Uchumi wa Kati inawezekana, wakati wa Mishahara naMaslahi bora kwa wafanyakazi ni sasa’. Maadhimisho Kitaifayamefanyika Mkoani Mbeya ambapo Mgeni rasmi ni Rais wa jamhuri ya Muungano waTanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara
Anuani ya Posta: 544, MTWARA
Simu: +255 23 2333014
Mobile: +255 23 2333014
Barua Pepe: ras@mtwara.go.tz
Haki Miliki © 2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara. Haki zote zimehifadhiwa.