Maafisa Utamaduni wa halmashauri za mkoa wa Mtwara wakifuatilia mjadala katika kikao kati yao na Maafisa wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) kilichofanyika jana Katika ukumbi wa Boma Mkoa ulioko Ofisi ya Mkuu wa mkoa Mtwara
Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) limewataka wasanii kote nchini kusajili kazi zao ili kupata fursa ya kutambuliwa na kutambulishwa katika taasisi mbalimbali. Akizungumza katika kikao kazi cha Maafisa Utamaduni wa halmashauri za mkoa wa Mtwara, Mratibu wa Sanaa Kanda ya Kusini Bona Masenge amesema serikali ya awamu ya tano imedhamilia kuhakikisha msaanii wa Tanzania anafanya kazi katika mazingira yanayomuwezesha kujiendeleza zaidi. ili hayo yote yawezekane inapaswa wasajiliwe na kutambuliwa.
Amesema mkakati wa Baraza la Sanaa la Taifa ni kuimarisha mahusiano ya kiutendaji kati ya wasanii, Baraza, mkoa, wilaya na Halmashauri kwa lengo la kuhakiksiha wanafanya kazi kwa ushirikiano.
‘Msanii anaposajiliwa anakuwa na faida ya kutambulika, BASATA pia inapata nafasi ya kumtambulisha kwa jamii na taasisi mbalimbali. hiyo itamsaidia kuwa karibu na wadau wa sanaa na kushikirikishana katika mambo mbalimbali.’ Amesema Masenge.
Kwa upande wake Afisa Utamaduni Mkoa wa Mtwara Fatuma Mtanda amsesema Mkoa uko tayari kutoa ushirikiano kwa wasanii wote hivyo wajitokeze kusajiliwa. amesema gharama za usajilli siyo kubwa hivyo hawana lolote la kuhofia. amewasisitiza Maafisa Utamaduni wa halmashauri kuhakikisha wanatimiza wajibu wao ili jamii iwaamini.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara
Anuani ya Posta: 544, MTWARA
Simu: +255 23 2333014
Mobile: +255 23 2333014
Barua Pepe: ras@mtwara.go.tz
Haki Miliki © 2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara. Haki zote zimehifadhiwa.