Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mhe. Gelasius Byakanwa akielezea fursa ya uwekezaji kupitia bidhaa zitokanazo na zao la korosho (Mvinyo wa Mabibo) kwa wawekezaji kutoka mataifa mbalimbali walipotembelea Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Naliendele Julai 13, 2019.
Wageni kutoka mataifa mbalimbali waliotembelea Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Naliendele wamepongeza kituo hicho katika jitihada zake za kuongeza Thamani ya zao la korosho. Wageni hao ambao walihudhuria kongamano la kimataifa la Uwekezaji katika sekta ya korosho wamesema uwepo wa Taasisi hiyo umeongeza mvuto kwa wekezaji hasa kutokana na utafiti wake ambao umezalisha bidhaa nyingi ikiwemo maziwa ya korosho.
akizungumza wakati wa tukio hilo Mkurugenzi wa kampuni ya Denia Holiday kutoka Morrocco, Mustapha Laraqvi amesema maziwa ya korosho yanayozalishwa ambayo pia yamefanyiwa utafiti kituoni hapo yanathamni kubwa na yanasaidia sana katika uchumi wa mataifa ya nje ikiwemo Marekani.
Anasema Tanzania wakiamua kujipanga sawaswa zao la korosho linaweza kusadia kwa kiasi kikubwa kukua kwa uchumi wa nchi.
Kutazama Video Bonyeza HAPA
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara
Anuani ya Posta: 544, MTWARA
Simu: +255 23 2333014
Mobile: +255 23 2333014
Barua Pepe: ras@mtwara.go.tz
Haki Miliki © 2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara. Haki zote zimehifadhiwa.