Thursday 26th, December 2024
@Vituo vya Afya na Vituo vya Muda vilivyotengwa Mkoani Mtwara
Wizara ya Afya kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais TAMISEMI na wadau imeandaa kampeni shirikishi ya kitaifa ya kutoa chanjo ya Surua Rubella kwa watoto wote wenye umri chini ya miaka mitano (Miezi 9-59) kuanzia tarehe 15 hadi 18 Februari, 2024.
Lengo mahususi la kampeni hii ni kuzuia na kupambana na ugonjwa wa Surua Rubella kwa kutoa chanjo kwa watoto wote wenye umri chini ya miaka 5 kutokana na ukweli kwamba watoto wenye umri chini ya miaka 5 ndo huathirika zaidi unapotokea mlipuko.
Kupitia kampeni hii ndani ya Mkoa wetu, watoto wapatao 172,062 wataongezewa kinga kwa kuwapatia chanjo hata kama walishapata chanjo hizo kupitia utaratibu wa kawaida wa huduma za chanjo kupitia kliniki. Niwaombe wataalamu wetu kutoa chanjo hizi kwa walengwa wote kwa upendo na kwa umakini mkubwa sana ili lengo la kuwakinga watoto dhidi ya ugonjwa wa Surua na Rubella litimie. Wajibu wetu kama viongozi, wazazi, walezi na wananchi kwa ujumla ni kuhamasishana na kuhakikisha tunajitokeza kwa wingi kuwapeleka watoto wetu kwenye vituo vya kutolea chanjo vilivyopangwa ili kuhakikisha kila mlengwa anafikiwa katika eneo husika, na tuwe mstari wa mbele kukanusha upotoshaji unaoweza kujitokeza dhidi ya kampeni hii au chanjo kwa ujumla wake.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara
Anuani ya Posta: 544, MTWARA
Simu: +255 23 2333014
Mobile: +255 23 2333014
Barua Pepe: ras@mtwara.go.tz
Haki Miliki © 2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara. Haki zote zimehifadhiwa.