Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Mhe. Kanali Patrick Kenan Sawala kwa naiaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan leo tarehe 26 Novemba 2024 amekabidhi Shilingi Milioni 100 ikiwa ni kwaajili ya ujenzi wa Msikiti mkubwa wa kisasa wa Masjid RawdhwaTandahimba.
“Ombi langu ni kwamba mchango huu uliotolewa na Mhe. Rais uwe baraka, uendelee kutuunganisha kwa maana kwamba zile kamati za ujenzi ziendelee kufanya kazi zao kwa uadilifu, matumizi ya fedha yawe ya wazi ili watu wasotengeneza maswali. Pia nitoe rai ya kuwa waadilifu kwa matumizi ya fedha zinazoendelea kupatikana kutokana na michango mbalimbali.” Alieleza Kanali Sawala
Katika taarifa iliyosomwa na Mwenyekiti wa kamati ya ujenzi wa msikiti huo, Imamu Salimu Muwanya ilieleza kuwa kutokana na ongezeko la watu ndani ya wilaya ya Tandahimba uongozi wa Bakwata uliona ni vema kujenga msikiti mkubwa ambao gharama yake ilikadiriwa kuwa Shilingi Milioni 400.
“Tukiwa tunaendelea na maandalizi ya ujezi kwa awamu ya kwanza, Uongozi na wajumbe wa kamati ya ujenzi wa msikiti tulifikiria kupeleka ombi la msaada wa fedha kwa Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, tarehe 15/03/2023 barua hiyo iliwasilishwa rasmi alipotembelea wilaya ya Tandahimba.
Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Jamaldin Salim Chamwi kwa niaba ya jumuiya ya waislamu mkoa wa Mtwara amemshukuru Rais Samia kwa mchango huo alioutoa na kuahidi kushikamana pamoja na viongozi wa serikali.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara
Anuani ya Posta: 544, MTWARA
Simu: +255 23 2333014
Mobile: +255 23 2333014
Barua Pepe: ras@mtwara.go.tz
Haki Miliki © 2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara. Haki zote zimehifadhiwa.