Tuesday 3rd, December 2024
@Mtwara
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Kassim Majaliwa Majaliwa anategemea kufanya ziara ya kikazi Mkoani Mtwara. ziara hiyo itaanza Februali 26 hadi Machi 02, 2018 ambapo Mheshimiwa Mjaliwa atatembelea Wilaya zote 5 za Mkoa wa Mtwara.
Pamoja na mambo mengine Mheshimiwa Waziri Mkuu anatarajiwa kuwa na vikao na watumishi wa Umma na mikutano ya hadhara, vilevile atakagua miradi mbalimbali ya maendeleo.
Mheshimiwa Majaliwa ambaye atapokelewa Mjini Masasi atakagua na kufungua miradi mbalimbali ya maendeleo wilayani hapo kabla ya kuelekea Wilayani Nanyumbu Jumanne ya tarehe 27.
Februali 28 Mheshimiwa Majaliwa atakuwa katika wilaya za Newala na Tandahimba kisha kuendelea na ziara katika wilaya ya Mtwara kuanzia Februali Moja hadi mbili.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara
Anuani ya Posta: 544, MTWARA
Simu: +255 23 2333014
Mobile: +255 23 2333014
Barua Pepe: ras@mtwara.go.tz
Haki Miliki © 2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara. Haki zote zimehifadhiwa.