Mkuu wa Chuo kishiriki cha SAUT tawi la Mtwara, Stella Maris (STEMMUCO) Padre Prof. Thadeus Mkamwa amewatunuku wahitimu 581 astashahada, stashahada na shahada ya kwanza katika mahafali ya 13 yaliyofanyika leo tarehe 16 Novemba 2024.
Mgeni rasmi katika mahafali hayo ambae ni Naibu waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Mhe. Doto Biteko amewaambia wahitimu hao kuwa vyeti watakavyopata pekee havitoshi kukabiliana na changamoto bali maarifa waliyonayo.
“Yawezekeana miongoni mwa wahitimu hawa kuna wengine hawana furaha kwani wanajiuliza nini kitafuata baada ya kuhitimu, nini kesho yao; maswali haya ni kawaida kwa wahitimu lakini nataka niwaambia wakati wote jihamasishe mwenyewe usimuangalie mwenzio. Iwekeni hofu nyuma, kuwa na mwelekeo chanya. Anza kwa namna yoyote inayofaa,nendeni mkajaribu.” Alieleza Dkt. Biteko
Mhe. Biteko aliwasihi wanaoendelea na masomo kuzingatia masomo na kujiepusha na migogoro ya aina yoyote; huku akisisitiza jamii kuwekeza kwenye elimu kwani ni nyenzo muhimu inayoweza kutatua matatizo ya jamii.
Miongoni mwa wahitimu 581 ni mwanafunzi mmoja pekee ndie aliehitimu Shahada ya Uchumi (Bachelor of arts in ecomonics).
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara
Anuani ya Posta: 544, MTWARA
Simu: +255 23 2333014
Mobile: +255 23 2333014
Barua Pepe: ras@mtwara.go.tz
Haki Miliki © 2017 Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara. Haki zote zimehifadhiwa.